AINA ZA BARUA
Zifuatazo ni aina kuu za barua zinazoandikwa mara kwa mara:
· Barua za
Kirafiki: Hizi ni barua wanazoandikiwa wazazi, marafiki, watani na
wajuani. Hizi zina uhuru mkubwa katika kuziandika. Hazidai utaratibu wa
pekee sana. Mtu huwa huru kuandika upendalo ilimradi halimvunjii mtu
heshima yake.
Barua ya aina hii huandikiwa marafiki, na jamii. Huwa
mwandishi anajuli kama kwa wale anaowaandikia kwa hivyo si lazima iwe na sahihi
yake au majina (yake yote) kamili. Kwa kawaida barua hii inaanza kwa salamu.
Huwa ina anwani ya mwandishi peeke. Mwishoni mwandishi huweza hata kuwatumia
salamu watu wengineo anaowajua na wanaomjua.
(i) Muundo wa
Barua ya Kirafiki
Shule ya Msingi kibo,
Sanduku la Posta 120,
MOROGORO.
Agosti 3, 2005
Kwa Baba mpendwa,
Ni matumaini yangu kwamba hujambo, tangu tulipoachana. Je,
majirani zetu huko nyumbani huwajambo? Mimi ni mzima, sina neno.
Madhumuni ya kukuandikia barua hii ni kukuarifu Maonyesho ya
Kilimo ya Wilaya ya Namtumbo. Kila mwanafunzi anahitajika kulipa shilingi mia
moja za kugharamia nauli, chakula na kiingilio. Nakuomba unitumie pesa hizi
tafadhali Baba, ili niweze kuandamana na wenzangu.
Nisalimie Mama, ndugu zangu na wote wanaonifahamu. Kwa heri
kwa sasa.
Ni mimi Kitinda-mimba wako,
Martha.
ZOEZI
1.
Wewe u mwanafunzi katika shule ya bweni. Mwandikie mama yako barua ya
kumjulisha siku ya kufungwa kwa shule, huku ukimuomba aje kukuchukua kwenda
nyambani.
2.
Umefuzu katika mtihani wako. Ndugu yako anayefanya kazi Nairobi, alikuwa
amekuahidi zawadi ,maalum, ukishapita mtihani huo. Sasa mwandikie barua,
umuombe akuletee zawadi.
3.
Umepata habari kwamba rafiki yako alipatwa na ajali ya barabara. Kwa sasa
amelazwa katika hospital kuu ya Mkoa wa Mashariki. Mwandikie barua ya kumpa
pole na kumtakia apone haraka.
4.
Likizo ya mwisho wa mwaka imekaribia. Mwandikie Baba yako anafanya kazi katika
nchi za mbali. Mwambie akuletee nguo mpya na aje kushiriki nanyi wakati wa
Sikukuu.
5.
U mwanariadha mashuhuri sana. Umechaguliwa kuiwakilisha shule yako katika
mashindano ya Wilaya. Mwandikie barua rafiki yako, umweleze vile ulivyoshiriki
na kupata ushindi katika mashindano ya Kata.
· Barua za
Mwaliko:
Unapoalikwa kwenye michezo, tafrija, mikutano
ya vyama au kwenye midahalo, unaandikiwa barua za mwaliko yenye sifa kama
ifuatavyo:
(i)
Barua hizi sharti ziwe fupi na wazi.
(ii) Zitaje
tarehe, saa na mahali pa kukutania;
(iii) Jina la mwalikaji na anwani yake
kamili lazima itajwe;
(iv) Aidha, jina la mwalikwa na kusudi la
mwaliko na pengine vitu anavyopaswa kwenda navyo inapaswa vitajwe.
· Barua za kazi na
shughuli:
Barua zinazohusika hapa ni zile za kuomba kazi, kutoa
ripoti ya kikazi, shughuli za kiserikali, kichama na kidini. Katika
barua hizi kumbuka:
(i) Kutaja nambari au/ na tarehe ya
barua zinazopaswa kurejewa;
(ii) Kichwa cha barua na aina ya shughuli
unayotaka izingatiwe.
· Barua ya Kiofisi
(Rasmi)
Barua ya aina hii huandikiwa Maafisa wa Serikali au
Makampuni ya watu binafsi. Kwa kawaida, maafisa hawa si lazima wamjue
mwandishi. Barua rasmi, basi huwa na anwani ya mwandishi (upande wa juu, mkono
wa kulia) na anwani ya anayeandikiwa, upande wa kushoto.
Anwani hufuatiwa na mtajo – (kichwa cha habari). Barua hii huanza moja
kwa moja, bila salamu.
Ujumbe pekee ndio unaoandikwa. Mwishoni, mwandishi huandika majina yake kamili
(rasmi) na sahihi yake.
(ii) Mfano/Muundo wa
Barua Rasmi:
Shule ya Msingi kibo,
Sanduku la Posta 222,
MWANZA
Agosti 3, 2005
Mkurugenzi,
Chama cha Wakuza Mboga,
Sanduku la Posta 456,
MWANZA
KUH: UUZAJI WA MBOGA
Ningependa kukujulisha ya kwamba Wanafunzi wangu wa Chama cha MOTCA wamekuza
kabichi na karoti nyingi.
Nakuomba utusaidie katika uuzaji wa mboga hizi ambazo kwa sasa tayari
zimekomaa.
Natumai utatusaidia uwezavyo.
Ahsante.
Wako mwaminifu,
(Sahihi)
Nsaji Peter Njarambaya
MWALIMU MKUU
Anwani
Kama mwandishi na mwandikiwa wote wanapatikana katika nchi
moja (Tanzania, Kenya, Uganda, Zimbabwe, Zambia, Malawi, nk.), basi anwani
huandikwa ndani ya barua kama ifuatavyo:
Shule ya Msingi kimawe,
Sanduku la Posta 2222,
moshi.
Agosti 3, 2005
lakini juu ya bahasha, yaani kule inakopelekwa barua,
huandikwa kama ifuatavyo:
Mkurugenzi,
Chama cha Wakuza Mboga,
Sanduku la Posta 56,
NAMTUMBO
Kama mwandishi na mwandikiwa wote wanapatikana katika nchi
tafauti (anayeandika yuko Tanzania, na anayeandikiwa yuko Kenya , Uganda
, Zimbabwe , Zambia au Malawi, nk.), basi anwani huandikwa ndani ya barua kama
ifuatavyo:
Shule ya Msingi Mawezi,
Sanduku la Posta 2222,
MWANZA.
TANZANIA
Agosti 3, 2005
na juu ya bahasha, yaani kule inakopelekwa barua, huandikwa
kama ifuatavyo:
Bwana
Paul Kipruto,
Chama cha Wakulima Langas,
Sanduku la Posta 146,
Eldoret,
KENYA
(iii) Mfano wa Bahasha
Bwana
Paul Peter Simala,
Chama cha Wakulima Mumias,
Sanduku la Posta 123,
Eldoret,
KENYA
· Barua za
Biashara na Matangazo: Matangazo ya biashara magazetini ni ghali. Kwa hivyo,
barua ziwe fupi na wazi ili zisimpotezee mfanyabiashara muda wake.
· Simu: Kuna simu
ya mdomo na barua ya simu. Barua za simu ni fupi sana. Mtu huna fursa ya
kueleza mengi au kuzungumza moja kwa moja na yule unayempelekea taarifa.
Isitoshe barua za simu zatarajiwa kwenda haraka zaidi kuliko barua za kawaida.
Gharama ya kuilipia hukadirwa kwa idadi ya maneno
yaliyoandikwa: maneno mengi, gharama kubwa, maneno machache, gharama ndogo.
Kwa ufupi, kuna barua ya kirafiki (kindugu) na barua ya
kiofisi (rasmi).
Hatua za Kuangalia katika Barua
Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa wakati wa kuandika barua ni
kama ifuatavyo:
(a) Hatua ya Jumla:
(i) Anwani ya
mwandikaji, ndani ya barua,
(ii) Anwani ya mwandikiwa
iandikwe vema, juu ya bahasha na pengine ndani ya barua pia;
(iii)
Tarehe,
(iv) Salamu (maamkio),
(v) Barua yenyewe,
(vi) mwisho wa barua.
(vi) Tumia karatasi na bahasha
safi.
(vii) Juu ya bahasha ya mtumiwa barua,
iwekwe stempu inayostahiki;
(viii) Kama ni kifurushi, funga kamba kwa umbo
la kukatana;
(ix) Iwapo ni rejesta, chora
mistari ya kukatana: moja wa wima na mwingine wa kulala katikati ya bahasha
nyuma na mbele.
(b) Hatua za Pekee:
(i) Katika Barua za
Kazi na Shughuli za Kiserikali:
Licha ya hayo yaliyotajwa katika (a) hapo juu,
· Andika kichwa
cha barua kinachotaja nia ya barua kwa sentensi
moja fupi kabla ya maelezo ya
barua yenyewe.
· Barua nzima iwe
fupi na wazi.
(ii) Katika Barua za
Biashara:
Pamoja na hayo yaliyotajwa katika (a) hapo juu,
· Ongeza orodha ya
vitu unavyoagizia.
· Eleza jinsi ya
kulipia iwapo ni kwa fedha taslimu, au malipo mara upokeapo vitu unavyoangiza
yaani, (c.o.d }ikiwa na maana ya: (‘cash on delivery’} au iwapo ni kwa hundi.
(iii) Barua za Simu
Mambo muhimu yanayotakiwa katika barua za simu ni:
· Anwani kamili ya
mtu yule unayempelekea simu.
· Toa taarifa kwa
kifupi na wazi kwa maneno yasiyozidi kumi.
· Kumbuka
maneno yote yanaozidi kumi ya kwanza utatozwa zaidi.
· Andika anwani ya
mtuma simu.
· Malipo taslimu
ya nayotolewa palepale posta.
(iv) Kutuma Fedha kwa Simu:
Ili kutuma fedha kwa simu zingatia mambo haya:
· Lipa fedha
taslimu kwa postamasta ofisini pamoja na ada ya kupelekea hizo fedha.
· Dai risti ya
kupelekea hizo fedha, nayo uitunze ili uweze kuitumia kudai pesa zako
hizo ikiwa zitapotea.
· Mwandikie
nduguyo unayempelekea hizo fedha ukimwarifu kwamba umemtumia fedha kiasi
kadhaa, ili atakapoitwa posta na kuulizwa nani amemtumia fedha hizo, aweze
kutaja jina lako na kupewa fedha zake.
(v) Kutuma Fedha kwa Barua ya
Rejesta:
Pamoja na kutumiwa fedha kwa njia ya simu, kupo pia
kupelekewa fedha kwa barua ya fedha au rejesta. Hapa yafaa kukumbusha tu kwamba
uchukuapo fedha zilizofika kwa rejesta, ifungue bahasha mbele ya postamasta na
kuhesabu kwa uangalifu pesa zilizomo mbele yake, ili zikipungua au zisipokuwamo
uweze kuanza madai mbele yake yeye akiwa shahidi.
(vi) Kutuma taarifa kwa njia
ya Faksi
Pamoja na simu leo kuna teknolojia za kisasa zaidi za
kupashana habari. Nazo ni: Teleprinta, Teleksi, Faksi na Intaneti.
Kwa mfano, ukitaka kutumia taarifa kwa faksi, njia ambayo
bado inayohifadhi siri kwa kiasi kikubwa, na inayochukua muda mfupi na gharama
ndogo ni faksi.
Unachotakiwa kukifanya
ni
· Kuandika taarifa
yako kikamilifu kwenye karatasi nyeupe.
· Kisha ipitishe
hiyo karatasi yenye taarifa yako kwenywe mashine ya faksi ambayo itaituma
taarifa yako huko unakotaka iende.
Huko iendako itapokelewa na faksi-mashine nyingine ambayo
itatoa kwa maandishi nakala halisi (kopi) ya taarifa yako ambayo ataipokea
uliyemtumia.
1.
Tarehe zinaweza kuandikwa kama ifuatavyo:
(a)
3, Agosti, 2005
(b)
3 – 8 – 2005
(c)
3/8/2005
2.
Anwani inaweza kuandikwa kama ifuatavyo:
(a) Shule la Msingi
Mbeya,
S.L.P. 343,
MBEYA.
au
(b) Shule ya Msingi
MBEYA,
Sanduku la Posta 343,
MBEYA.
TWITTER
TUNAKARIBISHA MATANGAZO
Copyright © 2015 Swahili form
Created By B - NATION Blogger Themes
No comments :
Post a Comment